Korea Kaskazini bado ianaonyesha kukaidi agizo la Umoja wa Mataifa na washirika wa Marekani kusitisha mpango wake wa majaribio ya silaha za Nyuklia baada ya hapo jana kufanya jaribio jingine la silaha za aina hiyo na kutoa taarifa kuwa limefanikiwa kwa asilimia 100.

Nchi hiyo imekuwa katika mvutano na Marekani pamoja na nchi jirani zikipinga vikali mpango huo wa majaribio ya silaha za nyuklia huku zikiuita mpango huo kuwa ni uchokozi dhidi ya nchi jirani na unahatarisha usalama wa dunia.

Katika kupinga mpango huo wa Korea Kaskazini, nchi ya Marekani imejitokeza hadharani kushawishi Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo nchi hiyo kwakuwa Rais Kim Jong-Un ameonyesha kukaidi huku akijitokeza hadharani kushuhudia majaribio hayo.

Kwa upande wake Rais Kim Jong-Un amesema kuwa jaribio la hivi karibuni limefanikiwa kwa asilimia 100 hivyo ameahidi kuendelea kufanya majaribio ya silaha hizo za Nyuklia

?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 15, 2017
Video: Katibu CCM auawa kwa risasi nne, Mali za kigogo zashikiliwa