Mchele wa Kyela, Mbeya ambao husifika sana kwa ubora wake huenda ukapoteza ubora wa kuingia kwenye soko la kimataifa kutokana na hatari inayotokana na kupakwa mafuta kwa lengo la kuuongezea mvuto.

Kwa mujibu wa mtaalam kutoka Staple Value Chain Activity inayojihusisha na kilimo cha mazao ya nafaka iliyo chini ya ufadhili wa USaid, Ladislaus Ikombe, mchele huo unapakwa mafuta kwa kuchanganywa katika mazingira machafu. Alisema kuwa waandaaji hutumia miguu kuuchanganya na mafuta katika chumba ambacho mazingira yake ni machafu.

Alisema kuwa mchele huo huwekwa mafuta kwa lengo la kuwaridhisha wateja ambao hutoka nchi jirani za Zambia na Somalia, lakini kitendo hicho kinaweza kuikosesha soko la kimataifa kwani unapopimwa hukutwa na mafuta mengi yasiyohitajika.

“Wanadai wanaweka mafuta kwenye mchele kwa ajili ya kuung’arisha na kuondoa ukungu, lakini kitendo hicho ni cha hatari kwa vile mchele ukipimwa ili uingie soko la kimataifa unaweza kukosa vigezo kama kuwa na mafuta yasiyo ya kawaida,” alisema Ikombe.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga alisema kuwa mamlaka hiyo haikubaliani na kitendo cha hicho na kwamba kuupaka mafuta mchele huo ni makosa.

 

Maalim Seif Ajitoa Akamatwe
Sababu Za Mama Regina Lowassa Kuikataa Ofa Ya Chadema Hizi Hapa