Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema kuwa atamchukulia hatua Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema baada ya kusambaza taarifa alizoeleza kuwa ni za uongo kuhusu mauaji ya watu 14 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza leo Machi 12, 2020, DPP Mganga amesema kuwa taarifa alizozitoa Lema zimeleta taharuki kwa Watanzania na kuwafanya wasiishi kwa amani na kwa jambo hilo lazima atalichukulia hatua.

“Tunapochukua hatua mnielewe, hatuwezi kuendelea kuwa Taifa la watu wenye uzushi, kwa hili nitachukua hatua, hatuwezi kuendelea kuwa na upotoshaji wa namna hii, halafu watu wanasema wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaonewa wakati wanafanya upuuzi”.Amesema Dpp Mganga.

Lema anadaiwa kutoa taarifa hizo Februari Mwaka huu, wakati akizungumza katika mazishi ya Katibu wa Chadema Singida Mashariki, Alex Joas ambaye mwili wake ulikutwa kando ya barabara ukiwa na majeraha kichwani.

Rais Magufuli amtolea Msigwa faini ya sh 38 Milioni
Mdee, Matiko, Bulaya watoka jela, Chadema walipa mamilioni 'walijua tunaenda jela'