Everton walienda sambamba na muda wa usajili uliofungwa rasmi jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki, kwa kumnasa moja kwa moja mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini England na klabu ya Tottenham, Aaron Lennon.

Everton wamemsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, baada ya kumchukua kwa mkopo mwanzoni mwa mwaka huu na sasa atakuwa huko Goodson Park kwa mkataba wa miaka mitatu.

Meneja wa The Toffees Roberto Martinez amesema ni faraja kubwa kuendelea kuwa na Lenon baada ya kuona umuhimu wake kwenye kikosi cha Everon kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Amesema aliweka nguvu zake zote kwa kuushawishi uongozi wake kufanya jitihada za kumsa mshambuliaji huyo, na sasa hana budi kushukuru kwa mipango yake kukamilishwa siku ya mwisho ya usajili.

Aaron Lennon alilazimika kuuzwa kwa mkopo baada ya mambo kuwa magumu kwake msimu uliopita kwenye kikosi cha Spurs na bado iliendelea kudhihirika hatokua na nafasi tena mara aliporejea White Hart Lane mwanzoni mwa mwa msimu huu.

Tonny Pulis Amuwekea Kauzibe Saido Berahino
Peter Msigwa, Lissu Wazungumzia Uamuzi Wa Dk. Slaa