Wahenga wanasema Adui yako muombee njaa ili ikimkamkata sana aje kuomba msaada lakini kauli hii kwa mwamuziki Linna Sanga ‘Linah limeonekana kutokuwa na uzito baada ya kumtakia aliyekuwa mpenzi wake baraka katika ndoa aliyoifunga hivi karibuni na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Khadija.

nagar-54-1

Ex- wa linah ambaye pia alikuwa meneja aliyeusimamia wimbo wa Olethemba Nagari Kombo ambaye pi alipata umaarufu mwaka 2010 alipoingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kumkumbatia Mchezaji wa Brazil, Ricardo Kaka waliachana mwaka jana baada ya kuwepo na tetesi za Wema Sepetu kuvamia penzi hilo.

Hivi karibuni Bw. Kombo alifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani alioneshwa kufurahishwa na tukio hilo huku akisema kuwa alishirikishwa na kukaribishwa katika tukio hilo alisema lina wakati akihojiwa na millard ayo entertainment.

”Mimi nina kitu kimoja nikishageuka nmegeuka na Ex wangu nilimpa baraka zote alinitumia sms akaniambia naoa karibu kwenye harusi, kwa sababu mimi na yeye tulifunga kurasa sioni sababu ya mimi kuendelea kumfuatilia au kumuombea mabaya kwani ndoa ni kitu kizuri na chenye baraka” -Linah

 

 

Video: Kamanda Sirro Azungumzia Sakata la Askofu Gwajima Kukamatwa Airport
Afanya ‘Honeymoon’ peke yake bila mume, kisa…