Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameanza kufanya mazoezi katika timu B na anaonekana anakaribia kupona kabisa. 

Kocha wa timu B, Gerard Lopez amesema kumekuwa dalili njema kutoka Messi ambaye amekuwa nje ya uwanja toka alipoumia goti katika mchezo dhidi ya Las Palmas Septemba 26 mwaka huu. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina anategemewa kuukosa mchezo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao Real Madrid Jumamosi hii kwasababu ya majeruhi lakini Lopez amebainisha Messi amekuwa akifanya mazoezi na kikosi chake na kuonyesha maendeleo mazuri. 

Lopez amesema Messi alikamilisha mazoezi na alionekana kutokuwa na tatizo lolote hivyo anadhani hizo ni dalili njema. Lopez aliendelea kudai kuwa anashukuru kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 kufanya nao mazoezi.

Bunge Laanza Moto, Nape Aambiwa Anasumbuliwa Na Utoto
Utafiti: Kujamiiana Kiasi Hiki Kutakuongezea Kinga Hii