Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, amepingwa vikali kuhusu agizo lake la kuwataka Mawakili kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili
Hayo yamesemwa na Wakili wa kujitegemea na Mmiliki mwenza wa Smile Stars Attorneys, Leonard Tungaraza Manyama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa yeye kama mwanasheria na mwanachama wa TLS, amesikitishwa na tukio la shambulio kwenye ofisi za IMMMA Advocates na kuitaka TLS kutoa muda kwa vyombo vya dola kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Aidha, Manyama amedai mawakili na wanasheria ni watumishi wa idara ya mahakama na kwamba tukio lolote la kutofanya kazi katika siku mbili hizo kutaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta haki zao kwa muda mrefu.
-
Hata mimi siwatambui akina Seif- Ndugai
-
Lema apigwa marufuku kufanya mkutano
-
Zitto ang’ata na kupuliza Serikalini
Hata hivyo, Tungaraza ameibuka siku moja baada ya Rais huyo wa TLS kuwataka mawakili kutohudhuria kwa siku mbili shughuli za mahakama Jumatatu na Jumanne kama ishara ya kulaani tukio la shambulizi lililofanywa kwenye ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu.