Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Machi 15, 2017 anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2016.

Makonda amesema kuwa anayofuraha kubwa kutimiza mwaka mmoja pamoja na changamoto mbali mbali katika kipindi hicho, amesema katika kipindi cha mwaka mwingine unaoanza atakuwa na kasi zaidi kwani amepata nguvu na ukomavu zaidi.

Makonda amesema kuwa yote yanayofanyika Dar es salaam, ni kwa upendo na wala si kwa chuki na mtu yeyote, amesema hayo yote ni kwaajili ya maendeleo ya wananchi wenyewe.

Spurs: Harry Kane Alijitonesha Jeraha La Mguu
Controversial Matters for Research Paper