Liverpool wameendelea na mikakati ya kutaka kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Arsenal, ili kukamilisha mpango wa kumsajili beki wa pembeni kutoka nchini England, Kieran Gibbs.

Gibbs mwenye umri wa miaka 26, msimu uliopita alikua na wakati mgumu wa kucheza mara kwa mara, kufuatia ushindani alioupata kutoka kwa beki wa nchini Hispania, Nacho Monreal.

Liverpool wameona kuna haja ya kumsajili Gibbs aliyekuzwa katika kituo cha kulelea vipaji kwa vijana cha Arsenal, kutokana na hitaji la beki wa kushoto ambalo linawakabili kwa sasa.

Hitaji hilo kwa The Reds, limekuja kufuatia mpango wa kumuweka sokoni beki wa pembeni kutoka nchini Hispania, Alberto Moreno.

Thamani ya Gibbs inakadiriwa kufikia Pauni milion 12, kutokana na kusaliwa na mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Arsenal, hivyo Liverpool kama watakubaliwa kufanya mazungumzo ya kumsajili beki huyo, wataanzia kiasi hicho cha pesa.

Azam FC Kugeukia Michuano Ya Vijana Barani Afrika
Cristiano Ronaldo Apigania Hatma Ya James Rodriguez