Chama cha soka nchini England (FA), kimetoa tahadhari kwa viongozi wa klabu za Liverpool na Man Utd kwa kuwataka wawakanye mapema mashabiki wao kuelekea katika mchezo wa siku ya jumatatu ambao utachezwa kwenye uwanja wa Anfiled.

FA wametoa tahadhari hiyo kwa kutumia kigezo cha vurugu zilizojitokeza wakati timu hizo zilipookutana mwezi Mei kwenye michuano ya kombe la Europa League, na kupelekea shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuzitoza faini ya Euro 40,000 sawa na Paundi 30,565, kufuatia vurugu zilizojitokeza katika michezo miwili ya hatua ya mtoano iliyochezwa Old Trafford na Anfiled.

Katika michezo hiyo mashabiki wa Liverpool waliwasha miale ya moto na kuitupa sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Anfiled ili hali wale wa Man utd walilipiza kisasi kwa kujazama katika kituo cha treni na kuzua tafrani kwa watu wengine waliokua na nia ya kuwahi kufanya shughuli zao.

Hata hivyo pamoja na FA kutoa tahadhari hiyo, tayari mashabiki wa pande zote mbili wameanza kuonyesha viashiria vya kuleta fujo kupitia mitandao ya kijamii, na suala kubwa linalojadiliwa ni uteuzi wa mwamuzi Anthony Taylor ambaye anadaiwa huenda akaibeba kwa makusudi Man Utd.

Kisingizo kikubwa kinachotumiwa na mashabiki wa Liverpool ni kwamba, mwamuzi huyo alizaliwa mjini Manchester na kwa sasa anaishi maili sita kutoka Old Trafford, hivyo inawaaminisha huenda akaamua kuipendelea timu ya nyumbani kwao.

Mashabiki wa Man Utd wamekua wakipinga suala hilo na kuwataka wapinzani wao kukaa mkao wa kula kwa kusubiri kichapo kama walivyowafanya msimu uliopita, ambapo Liverpool walifungwa katika mchezo wa nyumbani na ugenini.

Video: Diamond atoa msaada wa sh. mil. 2 kwa kijana aliyetobolewa macho na Scorpion
Vincenzo Montella Amkataa Cesc Fabregas AC Milan