Nyota wa zamani wa Bayern Munich, Lothar Matthaus amedai kuwa klabu hiyo ilimchukua Thomas Tuchel kwa ajili ya kuizuia Juventus isimchukue.
Bayern ilimtimua kocha Julian Nagelsmann, Machi mwaka huu, baada ya kuwa na mazungumzo ya dakika 61, wakati akiwafokea wachezaji wake kwa kutoonyesha jitihada kwenye mchezo wa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Ikiwa chini ya Nagelsmann msimu huu, Bayern ilipoteza mechi tatu pekee kati ya 27 kwenye ligi, wakati pia ikitinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Nafasi yake ilichukuliwa na Thomas Tuchel, kabla ya kubainika kwamba mazungumzo ya kumchukua kocha huyo wa zamani wa Chelsea yalianza siku tatu kabla ya kutimuliwa kwake.
Na Matthaus amekiri kushitushwa na uamuzi wa timu yake hiyo ya zamani kumtimua Nagelsmann haraka, wakati Tuchel alishatakiwa na Juventus.