Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameapa kuwa hataacha kujihusisha na masuala ya siasa huku akiwaambia wanaomshauri kupumzika tasnia hiyo, kuwa wamegonga mwamba kwani hafikirii hata kuacha uongozi katika chama chake.

Uhuru ameyasema hayo wakati wa kongamano la kitaifa la wajumbe wa chama cha Jubilee mapema Mei 22, 2023 na kuongeza kuwa si jambo la kushangaza wastaafu wakaendelea kulitumikia Taifa na hata kujihusisha mambo ya msingi katika jamii ikiwemo Siasa.

Amesema, “nawaambia wale ambao wanasubiri mimi kubanduka katika siasa au uongozi ni hivi wajameni mimi sitabanduka, hakuna dhambi yoyote kwa mimi kujishughulisha na siasa na ile mambo ya kuniambia eti acha siasa sitaacha hadi pale nitakapoombwa kufanya hivyo na chama changu.”

Aidha katika hatua nyingine Uhuru amesema Wakenya wote wanastahili heshima, na kwamba kukaa kwake kimya si udhaifu huku akiwataka viongozi wa Taifa hilo kufanya kazi kwa misingi ya haki na uadilifu ili waheshimiwe na jamii.

Jean-Jacques Ndala kuamua Benjamin Mkapa
Lothar Matthaus afichua siri nzito Bayern Munich