Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limemteuwa mwamuzi kutoka DR Congo Jean-Jacques Ndala Ngambo kuchezesha mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya USM Alger ya Algeria, utakaopigwa Jumapili (Mei 28), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mwamuzi huyo mwenye miaka 35, ni kati ya waamuzi wazoefu aliyechezesha mechi 34 za mashindano ya CAF tangu 2017, lakini ana uzoefu mkubwa na mechi za Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kwenye mechi hizo ameonyesha kuwa sio wa masihara kwani suala la kutoa kadi ni la kawaida, hivyo wachezaji wa Young Africans na Algers wanatakiwa kuwa makini zaidi, kwani amewahi kutoa za njano 98 na nyekundu tatu.

Ngambo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya RS Berkane dhidi ya Hassania Agadir ambayo Berkane ilishinda 2-1, alitoa kadi nane za njano. Mchezo mwingine aloitoa kadi nyingi za njano ni wa Ligi ya Mabingwa ambao Simba ilishinda 2-1 dhidi ya RSB aliotoa saba.

Pia ni kama vile ana kismati na timu za Tanzania kwani ameshachezesha mechi tatu za Simba huku mbili Simba ikifungwa na moja ikishinda, ambapo aliichezesha kwenye Shirikisho dhidi ya Saoura ambao Simba ilifungwa 2-0 mwaka 2019, na dhidi ya Galaxy, Simba ilipoteza 2-0 msimu uliopita. Mchezo wa mwisho wa Simba kuchezesha ni Ligi ya Mabingwa ambao Simba iliifunga RS Berkane 1-0 msimu uliopita.

Mechi nyingine alizochezesha Recreativo do Libolo vs Zesco (njano nne), Mamelod Sundowns vs Wydad Casablanca (alikaa mezani), Al Masry vs Songo (kadi ya njano moja) na FC Platinum vs Al Ahly (njano tatu).

Wydad Casablanca vs Mamelodi Sundowns (njano nne), Etoile du Sahel vs Zamalek (njano tano), RSB Berkane vs Gor Mahia (njano moja) na Saoura vs Simba (njano moja), Lobi Stars vs Wydad Casablanca (njano nne), Orlando Pirates vs CARA Brazzaville (njano moja), Etoile du Sahel vs De Agosto (njano mbili) na Mamelod Sundowns vs Togo Port (njano moja).

Galaxy vs Simba (njano mbili), Raja Casabalanca vs Kabylie (mwamuzi wa mezani), Kaizer Chiefs vs Wydad Casablanca (njano tano), Al Ahly vs RSB Berkane (mwamuzi wa mezani), Belouizdad vs Es Tunis (njano nne), Zamalek vs Es Tunis (njano nne) na Petro de Luan- da vs Wydad Casablanca (njano’ tatu).

RSB Berkane vs Hassania Agadir (njano nane), Al Ahly vs Mamelod Sundowns (njano moja), Al Nasry vs Horoya (njano nne) na ES Tunis vs Kabylie (njano nne).

Belouizdad vs Al Merreikh (njano sita), FAR Rabat vs Future (njano tatui), Mamelod Sundowns vs Al Hilal Omdurman (njano mbili na nyekundu moja), Coton Sports vs Royal Leopards (njanom mbili), Al Masr vs RSB Berkane (mwamuzi wa pembeni), Al Ahly vs Raja Casablanca (njano sita na nyekundu moja), Simba vs RSB Berkane (njano saba), Zamalek vs Petro de Luanda (njano tatu) na Al Ahly vs Raja Casablanca (njano nne).

Mohammed Kudus azivuruga klabu England
Mmegonga mwamba, sitaacha Siasa - Uhuru Kenyatta