Kiungo kutoka nchini Ghana Mohammed Kudus ameripotiwa kuweka wazi kuwa anataka kuondoka Ajax, huku ikitajwa kuwa yupo mbioni kujiunga na moja ya klabu za Ligi Kuu ya England.

Nyota huyo mwenye miaka 22 alikataa ofa ya kuongeza mkataba kuitumikia miamba hiyo ya Uholanzi, Aprili, na sasa amewaambia kuwa anataka kuondoka wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa Juni.

Baada ya kufunga mabao 22 kwenye michezo 48 aliyoichezea klabu na taifa lake msimu huu, kiungo huyo mshambuliaji amezitamanisha klabu nyingi za Ligi Kuu ya England.

Gazeti la The Athletic liliripoti kwamba Arsenal, Manchester United na Newcastle United zote zimeonyesha nia ya kumsajili raia huyo wa Ghana, ambaye ana mkataba na miamba hiyo ya Johan Cruyff Arena hadi 2025.

Mwezi Machi, iliripotiwa kuwa kocha wa zamani wa Ajax, Erik ten Hag alipanga kumsajili.

Tume ya uchunguzi mauaji ya Shakahola yapigwa stop
Jean-Jacques Ndala kuamua Benjamin Mkapa