Picha kutoka Maktaba, picha za Mwanza ndani ya habari:

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa jana alivunja rekodi katika jiji la Mwanza baada ya kukusanya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliofika katika viwanja vya Furahisha kumsikiliza akitafuta wadhamini, umati ambao unasadikika kuwa haujawahi kushuhudiwa jijini humo.

Lowassa ambaye aliambata na na viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa, alipata nafasi ya kuzungumza na maelfu ya wananchi hao na kutoa onyo ambalo linaweza kutafsiriwa kwa lugha ya vijana kuwa ‘mkwara’ kwa jeshi la polisi ambalo lilipiga mabomu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho katika eneo la uwanja wa ndege.

Alisema kama wataendelea na walichofanya watajikuta katika Mahakama Ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), The Hague baada ya uchaguzi mkuu.

“Nimesikitishwa sana kuwa watu wamepigwa mabomu asubuhi. Mkiendelea na mchezo huu tukimaliza uchaguzi tutawapeleka The Hague mkakipate cha moto na huko hamtarudi tena,” alisikika Lowassa.

mwanzaa

Lowassa pia alitoa onyo kwa Shirika la Umeme Mkoani Mwanza (Tanesco-Mwanza) kuhakikisha linakomesha tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara. Alimtaka mbunge wa Ilemela, Ezekiel Wenje kufuatilia tatizo hilo katika ofisi za Tanesco na kwamba endapo hataridhika na majibu watakayopewa ampigie simu.

mwanza mwanza

 

Lowassa alipokelewa kwa mbwembwe na maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao walifagia barabara na kudeki kila mara ili mgombea huyo apite sehemu safi zaidi. Msafara huo ukitumia muda mrefu kutoka uwanja wa ndege hadi katika viwanja vya Furahisha kwa kuwa ulilazika kutembea kwa mwendo wa kilometa takribani sifuri kwa saa kutokana na msongamano wa watu.

Jeshi la Polisi jijini humo lilieleza kuwa lililazimika kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya wananchama wa vyama vya Ukawa kwa kuwa walikuwa wamezuia shughuli za uwanja wa ndege kuendelea kwa muda kutokana na msongamano mkubwa.

Barcelona Kulipiza Kisasi Leo?
Nape: Viongozi wa CCM Wengine Watahamia Ukawa