Meneja wa klabu bingwa barani Ulaya FC Barcelona, Luis Enrique ana matarajio makubwa ya kupindua matokeo ya mabao manne kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa pili wa kuwania Spanish Super Cup utakaochezwa hii leo dhidi ya Athletic Bilbao.

FC Barcelona walilambishwa shubiri ya kutandikwa kipigo hicho cha mbwa mwizi mwishoni mwa juma lililopita, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania taji la Spanish Super Cup ambalo humaanisha ufunguzi wa ligi ya nchini Hispania.

FC Barcelona hii leo watakuwa nyumbani Camp Nou, wakihitaji kuonyesha maajabu ya dunia ya kushinda mabao matano kwa sifuri dhidi ya wapinzani wao Athletic Bilbao, ambao waliutumia vyema uwanja wa San Mames kwa ushindi mnene.

Enrique, amesema anakiamini kikosi chake kinaweza kufanya lolote na kwa wakati wowote, kutokana na aina ya wachezaji alionao, hivyo hana shaka na amewataka mashabiki kukaa tayari na kuyapokea matokeo yatakayo washangaza hii leo.

Amesema ilikua ni bahati mbaya kwao kukubali kufungwa mabao manne kwa sifuri katika mchezo wa mkondo wa kwanza, kutokana na makossa waliyoyafanya kwenye mchezo huo, na sasa wamesha jirekebisha kikamilifu.

FC Barcelona walipokea kichapo hicho baada ya kuushangaza ulimwengu kati kati ya juma lililopita, kufuatia ushindi wa mabao matano kwa mnne waliouvuna dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa kuwania Uefa Super Cup uliounguruma mjini Tbilisi nchini Georgia.

Di Maria Uso Kwa Uso Na Mashabiki Wa PSG
Picha: Lowassa Apiga ‘Mkwara Mzito’ Mwanza