Katika kuhakikisha kuwa jiji la Dar es salaam linabaki salama na uhalifu unapungua, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amewataka wakurugenzi wa Halmashauri za Kigamboni, Ilala, Ubungo Temeke na Kinondoni kuanzisha daftari la wakaazi ili kuweza kutoa urahisi wa kukabiliana na uhalifu.

Lyaniva ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuhusu hali ya sekta ya mawasiliano na utangazaji nchini, amesema kuwa ili kuweza kukabiliana na uhalifu ni lazima kila kata iwe na daftari la wakazi ili kuweza kurahisisha kudhibiti uhalifu wowote ambao unaweza kujitokeza huo.

Aidha, amesema kuwa ili kuweza kukabiliana na wahalifu wa mitandaoni ni lazima kuanzishwe huduma za utoaji elimu kuhusu matumizi bora ya mitandao ya kijamii na simu za mikononi kwa wananchi.

“Elimu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii na simu za kisasa za mikononi inahitajika kwa watumiaji ili kuweza kuepuka matatizo ambayo yanaweza kumpata mtumiaji husika kwani asilimia kubwa ya watumiaji hawaelewi matumizi yake,”amesema Lyaniva.

Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na faida kubwa inayopatikana kutokana na ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini ambayo inawezesha ukuaji wa kasi kwa sekta nyingine,lakini kumekuwepo na baadhi ya watu wachache katika jamii ambao wanatumia fursa hiyo vibaya.

Serikali yakanusha takwimu zilizotolewa na Gazeti moja hapa nchini
Video: LHRC wampongeza JPM, wataka Serikali iwachukuliea hatua waliotajwa sakata la makinikia