Mkuu wa Kanisa la Anglikana Sudan Kusini, Justin Badi anaongoza kundi la maaskofu ambao watasusia Ushirika Mtakatifu katika Kongamano la Lambeth la mwaka huu, wakipinga mwaliko wa viongozi wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Chini ya uangalizi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ushirika wa Makanisa ya Kianglikana (GFSA), maaskofu wamesema wataendelea kuketi wakipinga mabadiliko ya dakika za mwisho kwa hoja ya Azimio namba 1.10, linalothibitisha mtazamo wa Ukristo wa kweli kuhusu ushoga lililofikiwa katika mkutano mwaka 1998 likisema ushoga haukubaliki.
“Cha kusikitisha, baadhi ya majimbo yanarekebisha baadhi ya mafundisho ili yaonekane kuwa muhimu na kurahisisha uanafunzi kama njia ya kurudisha nyuma mahudhurio ya kanisa yanayopungua kwa kasi kutokana na vitendo vya ushoga,” amesema Askofu Mkuu Badi.
Hata hivyo amesisitiza kuwa, “Lakini kama wanafunzi, hatuambiwi katika Maandiko kumfinyanga Yesu katika sura yetu bali kubadilishwa daima na Roho kuwa mfano wake na ikumbukwe hii Lambeth ni mkusanyiko wa maaskofu wa Ushirika wa Anglikana na hufanyika mara moja katika miaka 10.”
Maaskofu hao, wanakusanyika kwa mwaliko wa Askofu Mkuu wa Canterbury, ambapo Mkuu wa sherehe wa Kanisa la Anglikana duniani atasali, kujifunza Biblia, kusikia mapambano na furaha ambayo kila mmoja anapitia katika mazingira yao ya ndani na kushughulikia masuala yanayokabili ulimwengu”.
Mkutano huo wa kumi na tano wa Lambeth unafanyika katika Chuo Kikuu cha Canterbury huko Kent na utaendelea hadi Agosti 8, 2022 ukiwa na mada isemayo “Kanisa la Mungu kwa Ulimwengu wa Mungu: Kutembea, Kusikiliza na Kushuhudia pamoja”.
Ushirika wa Anglikana umegawanyika tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, kutokana na suala la kuwekwa wakfu kwa mapadre mashoga ulikuwa ukifanyika waziwazi.
Mgawanyiko huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba Maaskofu wahafidhina walikusanyika Yerusalemu kwa ajili ya Kongamano la Kimataifa la Anglikana la Anglikana (GAFCON), mwaka wa 2008.