Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemtaka Rais Joseph Kabila kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa hatagombea urais kwa muhula wa tatu.
Kauli hiyo ya Maaskofu imekuja baada ya mkutano wao kutathamini hali ya kisiasa nchini humo huku kukiwa na shinikizo kutoka Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa
Aidha, hayo yamejiri wakati serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika wiki hii kushinikiza kujiuzulu kwa Rais Joseph Kabila.
Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa DRC umepangwa kufanyika nchini humo mwezi Disemba mwakani wakati upinzani wa nchi hiyo umekuwa ukidai kuwa Kabila, anapanga kuwania tena kinyume cha katiba.