Kim Kardashian ameeleza jinsi ambavyo anaamini atatakiwa kufanya kazi ya ziada baada ya kumpata mtoto wake wa pili Disemba mwaka huu.

Kim K amemueleza Ryan Seacrest katika mahojiano maalum kuwa mumewe Kanye West anadeka na anahitaji umakini wa hali ya juu wakati wote, na sasa atakapompata mtoto wake wa pili atakuwa na mtihani wa kuwapa umakini wote wawili.

“Mume wangu anahitaji ‘attention’, kila mtoto anahitaji ‘attention’, ninafanya kazi kwa bidii na nataka kumpa kila mmoja ‘attention’ anayostahili,” alisema Kim K.

Kim Kardashian na Kanye West wanatarajia kumpata mtoto wao wa pili ambaye ameshabainishwa kuwa ni wa kiume katika kipindi cha sikukuu ya Christmas. Mrembo huyo ameonesha kufurahishwa na hatua hiyo akidai kuwa mbili ni nambari ya maajabu.

 

 

Lowassa Kuibuka Na Mazito
Mwenyekiti wa Chadema Geita Auawa Kikatili