Huduma za usafiri wa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam zimeingia katika changamoto baada ya madereva wa mabasi hayo kufanya mgomo baridi.

Baadhi ya madereva hao walifanya mgomo huo baridi jana kushinikiza uongozi wa Usafiri wa Mwendo Kasi (DART) kuwaongezea mshahara kutoka shilingi 400,000 hadi 800,000 kama walivyokubaliana awali.

Mmoja kati ya madereva wa mabasi hayo, Abdul Abbas alisema muwa awali walikubaliana na uongozi huo kuwa utawaongeza mshahara kwa asilimia 100 kutoka shilingi 400,000 lakini wameshtushwa baada ya kukabidhiwa mkataba kusaini kuona kiwango kilekile cha pesa.

Mbali na hilo, madereva hao wameeleza kuwa mkataba waliopewa una mapungufu kwani imeeleza kuwa mfanyakazi ‘anaweza’ kupewa ‘bonus’ , hali inayomaanisha kuwa sio lazima apewe.

“Wametumia neno ‘anaweza’ kwa lengo la kutunyima haki ya kudai bonsai. Walipaswa kueleza wazi kuwa dereva atapata bonus endapo atazidi malengo,” alisema dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Kishija.

Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alitafutwa kwa njia ya simu lakini alikataa kulizungumzia suala hilo jana akiahidi kutoa taarifa kamili leo.

Hata hivyo, madereva hao walionekana kuendelea na kazi ya kusafirisha abiria.

Didier Kavumbagu Awapa Masharti Magumu Mbeya City
Video: Aeshi Hilaly hakubaliani na serikali kuwakata wabunge posho zao