Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka visiwani Zanzibar timu ya Mafunzo wazee wa Jela jela wameondoka Visiwani leo saa 9:00 za mchana kwenda DR Congo kuwafata wapinzani wao mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchi hiyo timu ya AS Vita Club kwa ajili ya mchezo wao wa marejeano wa Klabu bingwa Barani Afrika utakaosukumwa siku ya Jumapili.

Katika mchezo wa Awali Mafunzo walipigwa 3-0 nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Amaani mchezo uliochezwa tarehe 13 ya mwezi huu wa Februari.

Jumla ya wachezaji 18 walieondoka wa timu hiyo ya Mafunzo ambapo walikabidhiwa Bendera na Mwinyi Jamal Ramadhan kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, hafla ambayo ilifanyika Kambini kwao Magereza Wilaya ya Mjini Unguja ambapo pia Mwinyi aliwapa moyo na nasaha nyingi katika mchezo wao wa marudiano ili wapinduwe matokeo ya Awali ya 3-0.

“ Munakwenda huko Kongo Mujue munawakilisha Zanzibar yote, zingatieni nidhamu, mufate mafunzo mulofundishwa na walimu wenu naamini mtashinda”. Alisema Mwinyi.

Kwa upande wake Nahodha wa kikosi hicho Haji Ramadhan Mwambe mtoto wa Magomeni Mzalendo amewaahidi wazanzibar watalipa kisasi na kushinda ugenini kama walivofungwa wao uwanja wa Amaan dhidi ya AS Vita Club.

“ Tunajua tulipoteza nyumbani kwetu, lakini hata juzi Arsenal alifungwa nyumbani kwao na Barcelona, sasa na sisi tunatoa ahadi tutarudi na ushindi”.

Wachezaji 18 waliondoka kwa timu hiyo ya Mafunzo ni Khalid Mahadhi na Abdul Swamad, Juma Othman Mmanga, Abdul Rahim, Said Mussa, Kheir Salum, Said Mkadar, Abdul Malik Adam, wengine ni Mohammed Abdurahim, Ali Juma, Hassan Ahmada, Rashid Abdallah,Amour Abdallah, Sadik Habibu, Samih Haji Nuhu, Abdul aziz Makame, Ali Othman Mmanga na Haji Ramadhan Mwambe.

Timu ya Mafunzo waliondoka visiwani Zanzibar leo saa 9:00 mchan kwa kutumia ndege ya Ethiopia Air way ambapo usiku watalala huko Ethiopia , na kesho saa 3:00 za asubuhi wataendelea na safari yao kwenda DR Congo kuwavaa AS Vital Club siku ya Jumapili.

Video Mpya: Nzaya Don Ngosha Ft. Mirror - Achana na Mimi
Hongera Dk. Kikwete, ila unapozima moto wa Libya zikumbuke ‘Cheche’ za Zanzibar