Jumla ya Magaidi 3,858 wakiongozwa na Makamanda wakuu sita na wafuasi wao, huku12 wakiwa ni wa familia moja, wamejisalimisha kwa mamlaka za usalama nchini Nigeria huku Jeshi la nchi hiyo likitangaza kuwaua wapiganaji waasi 41.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi, Operesheni za Vyombo vya Habari vya Ulinzi, Meja Generali Bernard Onyeuko, imesema tukio la kujisalimisha linatokana na wanajeshi kutokata tamaa baada ya kushambulia ngome za magaidi wa Boko Haram na Jimbo la Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP).
Onyeuko amesema, Makamanda hao sita waliojisalimisha ni pamoja na Malam Mala Hassan (Wali), Ali Madagali (Munzur), Musa Bashir (Chifu Anur), Buba Dahiru (Munzur), Jafar Hamma (Kaid), na Abbali Polisawa.
“Kitengo cha anga cha OPHK mnamo Julai 11, kilifanya operesheni ya kuzuia ndege katika eneo la Tumbum Jaki na Tumbum Murhu karibu na Ziwa Chad katika Jimbo la Borno, na kuua zaidi ya watu 21 ambao ni magaidi,” amesema.
Amefafanuwa kuwa sema Julai 1-14, 2022, magaidi 3,858 wa Boko Haram ambao ni wanaume 505, na wanawake 1,042 huku watoto wakiwa 2,311 wamejisalimisha.
“Wengi walijitokeza katika eneo la Serikali ya Mtaa ya Dikwa, na zaidi katika barabara za Dikwa – Gamborou-Ngala, barabara ya Pulka – Gwale huko Borno na wengine waliuawa wakiwemo wanawake wawili ambao ni Hauwa Gambo na Khadija Dirsa.
Onyeuko amesema katika mkondo huo magaidi 42 waliuawa maeneo tofauti, 10 walikamatwa wakiwa na bunduki 17 aina ya AK-47, bunduki moja ya QTC, bomu 1 la RPG, bomba moja la RPG, mabomu matano ya kurusha kwa mkono, raundi 120 za 5.5mm na raundi 54 za risasi maalum za 7.62mm.
Kujisalimisha kwa watu hao kunakuja ikiwa tayari magaidi 42 wa Boko Haram wakizuiliwa na wanajeshi wa Operesheni ya Hadin Kai (OPHK), katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.