Siku ya sita ya Ziara ya Waziri wa Nishati January Makamba kwenye Mikoa 14 na Wilaya 38 imemfikisha kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda unapojengwa mradi mkubwa wa uzalishaji Umeme wa Maji wa Rusumo (Rusumo hydropower Project).

Mara baada ya kukagua mradi huo, Waziri Makamba amepata nafasi ya kuongea na Wanahabari kuhusu hali ya mradi huo ulipofikia ambapo amesema “Kasi ya Ujenzi inaendelea vizuri na uko kwenye asilimia 95, za kukamilika kwa mradi huo.”

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akijadiliana jambo na wataalamu kuhusu ujenzi wa umeme wa Rusumo Hydropower Project.

Amesema Kampuni hiyo itauza umeme wake kwa mashirika ya Umeme ya nchi tatu ambazo ni Rwanda, Burundi na Tanzania mradi ambao umefadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), na wafadhili wengine wa Maendeleo.

Hata hivyo Waziri Makamba ameongeza kuwa, “Tunautegemea mradi huu kuongeza uhakika wa umeme kwenye ukanda huu wa Ziwa Victoria, maana jawabu la matatizo ya umeme kanda ya Ziwa ni mradi huu.”

Waziri waNishati, Januari Mkamba akikagua ujenzi wa mitambo ya umeme wa Rusumo Hydropower Project unaotarajiwa kukamilika Novemba 2022.

Mradi wa Rusumo Hydropower unatarajiwa kukamilika Novemba 2022  ukihusisha nchi 3 ambazo ni Tanzania, Rwanda na Burundi.

Magaidi wajisalimisha Jeshini, 12 wa familia moja
Kenya, Somalia zarejesha uhusiano baada ya mvutano