Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 16, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi na kuweka jiwe la msingi la kituo cha Afya cha Mtoa kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida.

Kituo hicho kitahusisha ujenzi wa majengo ya Mama na Mtoto, Jengo la Upasuaji, Jengo la
Maabara, Jengo la Kufulia, Jengo la Kuhifadhi Maiti na Nyumba ya Mtumishi.

Kabla ya ujenzi wa kituo hicho, huduma za afya kwa ngazi ya kituo cha afya zilikuwa
zikipatikana Shelui, ambako ni umbali wa kilomita 15.

Ujenzi wa kituo hicho ambao mpaka sasa umefikia asilimia 75, unategemewa kugharimu shilingi milioni 662.

Uviko-19 yavuruga utoaji chanjo kwa Watoto
Serikali kuhakiki maeneo ya shule na kuyapa hatimiliki