Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli,amefanya mabadiliko ya uongozi ndani CCM baada ya kuwateua wajumbe watatu wa Sekretarieti ya Chama hicho kuwa mabalozi.

Mabadiliko hayo yamekuja mara baada ya kuwateua wajumbe hao wa sekretarieti ya chama hicho kuwa mabalozi,Wajumbe Sekretarieti walioteuliwa ni pamoja na Pindi Chana, Emmanuel Nchimbi na Rajabu Omar Lwihavi, hali ambayo imesababisha nafasi zao kuwa wazi ndani ya chama.

Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi sita watakao iwakilisha Tanzania katika balozi mpya ambazo zitafunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki.

Walioteuliwa ni pamoja na Balozi Mbelwa Kairuki, Balozi Samuel Shelukindo, Balozi Joseph Sokoine, Balozi Silima Haji, Abdallah Kilima, Baraka Luvanda, Dkt.James Msekela na Balozi Mteule Sylivester Ambokile.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameteua mabalozi wengine 15 ambao vituo vyao vya kazi vitatajwa hapo baadaye na waliosalia kwenye vituo vyao wataendelea na nafasi ao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.

Tanesco yakamilisha baraka ya Rais Magufuli kwa Bakhresa
Justine Zullu Amkimbiza Mbuyu Twite Jangwani