Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa tatizo la umeme linaloendelea nchini limesababishwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

Mgombea huyo wa CCM aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana mkoani Lindi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho, ambapo alisema kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ndio chanzo cha tatizo la umeme nchini kwa kuwa ‘walipiga deal’ kupitia makampuni ya ufuaji umeme.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli aliwaeleza wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuwa atakapoingia madarakani atahakikisha wananchi wa eneo hilo wanafaidika na gesi kwa kuwapa kupata ajira kwa asilimia kubwa zaidi ya wale wanaotoka nje.

“Kwa wawekezaji watakaokuja kujenga viwanda vya gesi katika eneo la Mtwara na Lindi, wafanyakazi watakaokuwa wanafanya kazi katika viwanda hivyo kwa asilimia kubwa lazima watoke Lindi na Mtwara. Ili tuongeze ajira kutoka asilimia 9 mpaka asilimia 40. Haiwezekani viwanda hivi tunavyovijenga, dereva atoke Ulaya, mpishi atoke Ulaya, muuza mchicha atoke Ulaya,” aliongeza.

CCM Wampania Lowassa, Watosa Kukutana Na Wagombea Wengine
Jst Kidding: Young Dee asema Irene Uwoya ni Mpenzi Wake