Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameongoza mapokezi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mapokezi hayo, yamefanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar leo tarehe 02 Oktoba, 2020 ambapo Dkt. Magufuli ameeleza kwa ufupi.

“Leo nimeingia hapa Zanzibar, nimeingia Zanzibar kwa ajili ya kuja kufanya Kampeni, kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi.”

Mgombea wa Urais wa CCM Mhe. Dkt. Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano wa kampeni kesho tarehe 3 Oktoba, 2020 katika viwanja vya Mnazi mmoja Mkoa wa Mjini.

Hii hapa Taifa Stars itakayowakabili Burundi
KMC FC yatoa wachezaji wawili Taifa Stars