Mahakama Kuu nchini Afrika kusini imesema kuwa bunge la nchi hiyo halikutimiza wajibu wake ipasavyo kwa kushindwa kumuwajibisha Rais Jacob Zuma kuhusu madai ya ufujaji wa mamilioni ya dola zilizotumika kurekebisha na kupamba jumba lake la Nkandla.

Mahakama hiyo imesema kuwa pamoja na bunge la Afrika kusini kufanya kikao cha maswali na majibu kuhusu kashfa hiyo na hata kupigia kura mswaada wa kutokuwa na imani lakini hatua hizo zote hazikuwa na tija ya kumuwajibisha Rais Zuma.

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo Jaji, Chris Jafta amesema kuwa bunge ni sharti wakati wote litimize wajibu wake wa kumuwajibisha rais bila ya kuchelewa.

Hata hivyo, Chama tawala cha Africa National Congress kimetoa taarifa kikisema kuwa kitauangalia kwa makini uamuzi huo wa mahakama Kuu na kujadili kikamilifu athari za uamuzi huo katika kikao kamili cha baraza kuu la chama tawala katika muda wa wiki mbili.

 

Picha: Zitto aanika madeni na rasilimali zake
Trump ainyooshea kidole China