Wakati mapigano yakizidi kushika kasi nchini Sudan, umoja wa mataifa unasema jumla ya dolla bilioni 3.03 zinahitajika ilikutoa msaada wa dharura kwa raia walioathirika na makabiliano hayo.
Ripoti hiyo ya umoja wa mataifa, inakuja wakati huu raia zaidi ya milioni moja wakitarajiwa kutorokea katika mataifa jirani mwaka huu kutokana na mapigano kati ya Makundi mawili ya kijeshi.
Aidha, uhitaji umeripotiwa kuongezeka tangu kuzuka kwa mapigano mwezi uliopita, huku UN ikisema imeilazimu kufanya upya tathmini ya mpango wake wa kuisaidia Sudan.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika makao makuu ya UN mjini Geneva, watu 25 milioni nchini Sudan wanahitaji msaada wa kibindamu na ulinzi ili kujikwamua ma madhila yanayowakabili.