Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Al Ahly ya Misri Mahmoud Kahraba ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Wiki wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kupata kura 125,177 kati ya Kura 254,462 zilizopigwa.

Kahraba ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo hiyo kwa kupata asilimia 49% ya kura zote zilizopigwa kuanzia Jumanne (Machi 21) jana akiwashinda Clatous Chama na Sadio Kanoute wote wa Simba SC pamoja na Percy Tau wa Al Ahly.

Kahraba aliiwezesha Al Ahly kushinda mabao 4-0 dhidi ya Cotton Sport huku akifunga mabao matatu ‘Hat Trick’ (Bila Penati) na kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Kwenye kura zilizopatikana, Clatous Chama amepata asilimia 43% ya Kura zote zilizopigwa huku Percy Tau akipata asilimia 5% na Sadio Kanoute akishika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 2% ya Kura zote zilizopigwa katika ukurasa mtandao wa Twitter.

Mahmoud Kahraba anachukua utawala wa Chama aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki, baada ya michezo ya mzunguuko wanne wa Hatua ya Makudi Michuano ya vilabu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Ihefu FC yaitangulia Simba SC ASFC, Ligi Kuu
Sakata la Kapombe, Tshabalala latinga TFF