Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wote, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi watoe taarifa za fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi badala ya kusubiri ziara za viongozi wakuu.
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye kikao kilichofanyika Mbamba Bay, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
“Kuanzia sasa ninaagiza, viongozi wote wa ngazi za juu wakiwemo Mawaziri hadi Wakurugenzi na hata ninyi wakuu wa idara mnawajibika kutoa taarifa za fedha tunazopeleka kwenye miradi kwa sababu wananchi wana haki ya kujua utekelezaji wa ahadi za Serikali,” amesema Majaliwa
Amesema kuwa kila wanapoenda kwenye ziara ya kikazi vijijini, waelezee thamani za kazi zilizofanyika na waeleze ni lini miradi hiyo itakamilika.
Hata hivyo, amesema kuwa wananchi wana haki ya kupatiwa taarifa za utendaji wa Serikali yao na akawataka viongozi hao wasisubiri ziara za viongozi wa kitaifa.
-
Makonda ajitolea kujenga nyumba ya mwandishi
-
JPM amjulia hali Mzee Kingung’e Hospitali ya Muhimbili
-
Waliojiuzulu ubunge wateuliwa na CCM