Watu wanne wamefariki na wengine ishirini na watano wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyohusisha daladala (DCM) yenye abiria pamoja na maroli mawili, mapema leo jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo imeripotiwa kutokea katika eneo la Tabata Matumbi ambapo mashuhuda wameeleza kuwa daladala linalofanya safari zake kati ya Ubungo na Gongo la Mboto liligongana maroli mawili, moja likiwa la mizigo na jingine likiwa limebeba ng’ombe waliokuwa wakipelekwa  mnadani eneo la Pugu jijini humo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana amethibitisha kupokea wahanga wa ajali hiyo ambapo ameeleza kuwa wanne walifariki dunia na ishirini na watano wanaendelea kupata matibabu huku wengine wakihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Haya ni majina ya wahanga wa ajali hiyo waliofikishwa katika hospitali ya Amana mapema leo asubuhi. Tuendelee kuwaombea.

Majina ya Waliopata ajali

Ajabu: Apewa ujauzito na wanaume wawili, azaa mapacha wa baba tofauti
Boban, Kenny Ally Kuikosa Stand United