Liverpool inazidi kukwea vidato kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga Sunderland 1-0 katika mchezo uliochezwa Jumatano usiku.

Bao pekee la Liverpool lilifungwa na Christian Benteke sekunde chache baada ya mapumziko. Kwa ushindi huo Liverpool sasa imesogea hadi nafasi ya saba, pointi moja nyuma ya Crystal Palace iliyoko nafasi ya tano.

Lakini ushindi huo unaifanya Liverpool ifungane pointi na  Manchester United inayoshikilia nafasi ya sita.

Lionel Messi Acheza Game Ya 500 Akiwa Barcelona
Kamanda Kova Aliaga Jeshi la Polisi, Kustaafu rasmi leo