Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa ni vema rasilimali za nchi hii zitunzwe kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Amesema kuwa Ofisi yake ya imedhamiria kulichukulia kwa uzito wa kipekee suala la mazingira ikiwa ni pamoja na kuweka hifadhi ya mazingira katika mipango ya maendeleo.

Makamba ameyasema hayo mkoani Tanga ikiwa ni siku yake ya tano katika ziara anayoifanya mkoani humo  kwa ajili ya ukaguzi wa mazingira.

Aidha, Makamba ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji Korogwe kuwachukulia hatua kali wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kwa kutumia sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na ile ya maji ya mwaka 2009.

Vile vile, Makamba amesema kuwa Ofisi yake iko katika hatua za mwisho za kuteua wakaguzi wa mazingira 200 ambao watapata mafunzo na kusambazwa katika Halmashauri mbali mbali nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo, Hillary Ngonyani amesema kuwa katika kutekeleza sheria ya mazingira zoezi la uzoaji na utupaji wa taka ngumu na taka maji umewekewa mkakati maalumu na kutekelezwa kikamilifu pia usafi wa mazingira umefanyika kwa kufanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kutoza faini kwa wananchi wasio na vyoo.

Hata hivyo, Ngonyani ameinisha changamoto zinazojitokeza katika Halmashauri ya Korogwe Mji kuwa ni pamoja na Ukosefu wa wakaguzi wa Mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha vipindi vya mvua kubadilika na kuongezeka kwa joto

Maafisa habari watakiwa kutangaza mafanikio ya miradi
Magazeti ya Tanzania leo Machi 25, 2017