Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 08 Machi 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal Holding )
Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani Mazungumzo yaliofanyika katika Mji wa Doha nchini Qatar.

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amemkaribisha mwekezaji huyo nchini Tanzania kuwekeza katika fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ikiwemo katika miundombinu ya utalii kama vile Hoteli. Pia
Makamu wa Rais amesema Tanzania inayo fursa katika uwekezaji wa viwanda vya dawa , kilimo pamoja na madini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu ya Al
Faisal (Al Faisal Holding ) Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani Mazungumzo yaliofanyika katika Mji wa Doha nchini Qatar Machi 8, 2023.

Kutokana na serikali kuhamishia shughuli zake katika makao makuu ya nchi mkoa wa Dodoma, Makamu wa Rais amesema mkoa huo unayo fursa ya kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za makazi, hospitali pamoja na hoteli.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kampuni Tanzu ya Al Faisal (Al Faisal Holding) Sheikh Faisal Bin Qassim Al Thani ameahidi kufanya ziara nchini Tanzania pamoja na ujumbe wake ili kushiriki majadiliano ya pamoja katika kuangazia maeneo muhimu ya uwekezaji ikiwemo elimu, afya na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo.

Mkutano LDC5 waangazia mchango wa wanawake Kiteknolojia
Nabi atetea maamuzi ya kumtoa Aziz Ki