Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, amesema matukio ya wizi mdogo mdogo wa vitu kama ‘power windows’ yameongezeka na kumtaka Kamanda wa Polisi kuhakikisha hali inakuwa sawa.

Amesema, oparesheni maalumu ya kushughulikia Vibaka hao jijini Dar es salaam imeanza rasmi ambapo amemtaka kila mzazi kuhakikisha anamchunga mwanae kwakuwa hakuna kibaka atakaesalimika katika msako huo.

Amefafanua kuwa “Uibe tecno au pochi haina kitu tutakuhesabu kama mwizi wa Dreamliner, kipigo chako ni cha Kimataifa. Wale mnaotaka kuonja nafasi ya ukibaka kama ni nzuri onjeni na tusilaumiane, hakuna mtu yuko tayari kuharibiwa kazi kwenye hiki kipindi cha mwisho tunafunga mahesabu”.

Amemuelekeza Kamanda wa Polisi kuhakikisha wanawashughulikia ipasavyo vijana walioanza tabia ya kupora na kuiba Mali jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya watu.

Young Africans washindwe wenyewe kwa Andréa Fileccia
Mashabiki Benfica washambulia wachezaji