Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza benki zote zenye akaunti  zilizopokea mishahara ya watumishi hewa kurejesha fedha zote zilizopitia katika akaunti hizo ndani ya siku 21.

Makonda amezilima barua benki hizo akitoa masharti kuwa endapo hazitaweza kurejesha, zibainieshe majina ya waliokuwa wakitumia akaunti hizo kuchukua fedha.

Mkuu huyo wa Mkoa alieleza uamuzi huo hivi karibuni alipozungumza na waandishi wa habari jijini humo, ambapo alizitaja Benki na fedha ambazo zinadaiwa akisema ndizo zinazoweza kusaidia kuwabaini waliofaidika na mishahara ya watumishi hewa.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, Benki hizo ni pamoja na NMB inayodaiwa shilingi bilioni 2, CRDB zaidi ya shilingi milioni 400, NBC shilingi milioni 141, DCB milioni 85, Standard Chartered shilingi mkilioni 2 na Community Bank zaidi ya shilingi milioni 100.

“Tayari tumeshaziandikia benki hizo barua na kuwapatia majina na akaunti na kuwataka kutuwasilishia majina ya wahusika, waliohusika na akaunti hizo ili kusaidia kutambua mtandao mzima wa wahusika wa suala la watumishi hewa ambao wameigharimu serikali,” alisema Makonda.

Makonda aliagiza Benki hizo kufunga huduma za akaunti hizo hadi zitapokamilisha utatuzi wa sakata hilo la mishahara hewa na fedha hizo kupatikana.

CCM yatoa tamko kuhusu Kitwanga na kama itamuadhibu tena
Chadema: Mtu Pekee wa Kumsaidia Magufulini ni Lowassa