Timu ya taifa ya vijana ya Mali chini ya umri wa miaka 17 imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya AFCON U-17 mara baada ya kuitandika timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Ghana goli 1-0.

Aidha, mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika nchini Gabon yamemalizika kwa timu ya Mali kutawazwa kuwa mabingwa wa mashindano AFCON U-17 ya Afrika chini ya umri wa miaka 17.

Katika ushindi huo, bao pekee la Mali lilifungwa na Momadou Samake na kuihakikishia Mali kutetea ubingwa huo.

Kwa upande wake kocha wa Ghana, Paa Kwesi Fabin amesema kuwa alipanga kikosi chake cha kwanza ambacho kiliifunga Niger 6-5 katika hatua ya penalti kwenye hatua ya nusu fainali.

Hata hivyo, Kocha huyo ameongeza kuwa pamoja na kupoteza mchezo huo, wachezaji wake walifanya jitihada za kutosha ila bahati haikuwa upande wake

WCB wapigwa marufuku kuingia klabu usiku
Korea Kaskazini Yaichafua Japan kwa Kombora, Yazidi Kuivuruga Marekani