Korea Kaskazini imeendelea kuonesha ukaidi dhidi ya makatazo ya Marekani na Umoja wa Mataifa kwa kufanya majaribio mengine ya makombora ambayo yamethibitika kufanikiwa.

Kwa mujibu wa BBC, makombora yaliyofyatuliwa na Korea Kaskazini mara tatu mfululizo yalienda umbali wa kilomita 450 juu kabla ya kutua kwenye maji ya bahari ya Japan ndani ya dakika sita, hali iliyosababisha Japan kupinga vikali kitendo hicho.

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Japan, Yoshihide Suga ameviambia vyombo vya habari kuwa makombora hayo yalitua katika maeneo kati ya Sado na visiwa vya Oki, maeneo ambayo ni kanda muhimu za kiuchumi.

Wataalam wameeleza kuwa majaribio hayo ya hivi karibuni yanaonesha dhahiri kuwa Korea Kaskazini inapiga hatua nzuri katika kufanikisha makombora yake kubeba vichwa vya nyuklia.

Marekani imeendelea kuionya Korea Kaskazini ikiitaka isijaribu kucheza na moto kwani haitavumilia. Rais Donald Trump alilaani na kutoa onyo kwa tamko la Korea Kusini kuwa makombora yake ya nyuklia yanaweza kufika katika baadhi ya sehemu za dunia ikiwa ni pamoja na majimbo kadhaa ya Marekani.

Korea Kusini imekuwa ikijitetea kuwa program yake ya silaha ni muhimu dhidi ya vitendo vya ukandamizaji vya Marekani.

Mali watetea ubingwa wao AFCON U-17
?Live Ikulu: Rais Magufuli akimuapisha Simon Sirro kuwa IGP