Mama mzazi wa Kim Kardashian, Kris Jenner amesimulia tukio lililomuabisha zaidi kwenye maisha yake pale mhudumu wa ndege alipomuumbua baada ya kufanya mapenzi na mumewe Bruce Jenner ambaye sasa anaitwa Caitlyn Jenner, wakati chombo hicho kikiwa angani.

Katika kipande cha video kinachoonesha nyuma ya pazia kutoka kwenye ‘Cosmopolitan’s 50th Anniversary’, mama huyo anaeleza kuwa yeye na mumewe walikata tiketi ya daraja la kwanza na walipokuwa hewani waliingia bafuni na kufanya mapenzi.

Hata hivyo, wakati wanarudi na kukaa kwenye nafasi zao, ndipo mhudumu alipowaumbua kwa kutangaza kupitia kipaza sauti huku akiwapongeza kwa kusafiri na ndege hiyo.

Tukio hilo lilimfanya asikie aibu iliyopitiliza na ilimkera kiasi cha kutamani apotelee chini ya kiti.

“I could not squish down in my seat low enough. I was mortified,” alisema Kris Jenner.

Siri Ya Urafiki Wa Mrema Na Magufuli Hii Hapa
Huyu Ndiye ‘Star’ Aliyevunja Rekodi Ya Instagram Duniani