Beki wa kati wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho, ameongeza matumaini ya kuachana na klabu hiyo utakapofika wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka 2017.

Kwa mujibu wa jarida la soka la France Football, beki huyo ambaye hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Liverpool tangu mwanzoni mwa msimu huu, ameonyesha kuchoshwa na mwenendo huo.

Sakho, amekua hana maelewano mazuri na meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, kuanzia kipindi cha maandalizi ya msimu yaliyofanyika nchini Marekani mwezi July, ambapo beki huyo alidaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu wakiwa kambini.

Wakiwa kambinu Sakho aliwahi kuchelewa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake, na suala hilo lilimkera Klopp na kufikia hatua ya kumfukuza kambini kwa kumuamuru arejee nchini England.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, tayari ameshaitumikia Liverpool katika michezo 80, tangu aliposajiliwa mwaka 2013 kwa ada ya Pauni milioni 18 akitokea Paris Saint-Germain.

Wachina Wakaribia Kuinunua Southampton FC
Aliyemchinja mkewe na kutoweka ajisalimisha apate ARV