Meneja wa Brentford, Thomas Frank amethibitisha mabosi wa timu yake wapo tayari kumuuza Mlinda Lango wao, David Raya katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini ikiwa timu inayohitaji italipa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.

Mlinda Lango huyo kutoka Hispania amekuwa akihusishwa na Manchester United ambayo inamuangalia kama mrithi wa David de Gea ambaye kiwango chake kwa siku za hivi karibuni kimeshuka.

Raya mwenye umri wa miaka 27, pia ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Brentford ili kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa kwa msimu ujao.

Mbali ya Man United kipa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani huduma yake pia inahitajika na Chelsea ambayo pia ina upungufu kwenye eneo la golikipa.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Raya amecheza mechi 38 akiwa na Brenford na ameruhusu mabao 47 na kwa sasa ameisaidia timu hiyo kuwa nafasi ya tisa lakini ikishinda mechi yake ya mwisho na Aston Villa na Tottenham zikipoteza itaweza kufuzu European Conference League.

Mzozo wakulima, wafugaji wauwa 10, watuhumiwa mbaroni
Madai Polisi kuuwa raia sita: IPOA yaanza uchunguzi