Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ambaye anamaliza muda wake na anaomba kura za kuendele kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Januari 29, Murtaza Mangungu amekiri kuwa basi la timu hiyo limeuzwa na sio bovu kama inavyoelezwa.

Simba ambayo ni muda sasa basi lao limekuwa halionekani huku wakitumia basi dogo ‘Coaster’ na taarifa ya awali ikithibitisha kuwa basi ni bovu sasa imethibitika kwa limeuzwa.

“Nashushiwa lawama ambazo sio zangu basi la Simba limeuzwa mimi nikiwa sipo kwenye uongozi sikuwa Mjumbe wa Bodi wala Mwenyekiti wa timu hii kama nilivyo sasa,”

“Lakini baada ya kuingia kwenye uongozi hili suala lilipelekwa kwenye Bodi ya klabu na wajumbe tumelifuatilia na kubaini kuwa limeuzwa kwa kufuata utaratibu,” amesema Mangungu kiongozi huyo ambaye anaiongoza timu hiyo hadi Januari 29 ambayo ni siku ya uchaguzi mkuu.

Mangungu anatetea nafasi yake klabuni hapo sambamba Moses Stewart Kaluwa, baada ya Kamati ya Uchaguzi kuwapitisha wawili hao kuwania nafasi ya Mwenyekiti upande wa Wanachama.

Uviko-19: Wizara ya Afya kuzindua dozi ya nyongeza
Ahmed Ally: Tumefurahia maamuzi ya Kocha