Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Mfanyabiashara, Yusuph Manji katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili na kufuta kabisa kesi hiyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP ) amesema hana nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ndiyo sababu iliyofanya Hakimu kumuachia huru Manji kwani hakuna tena shtaka lililokuwa linamkabili.
Aidha, Yusuf Manji na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kukutwa wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni 192.5.
Hata hivyo, Julai 5, 2017, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ililazimika kuhamia kwa muda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kumsomea mashtaka 7 ya Uhujumu Uchumi Yusufu Manji alipokuwa akipatiwa matibabu na wenzake watatu.