Daktari wa  Hospitali ya Bugando, Dk.Cloud amewatoa hofu wananchi kuhusiana na hali ya mshereheshaji Emmanuel Matebe Mathias maarufu kama Mc Pilipili washawasha.

Daktari amesema kuwa hali ya Mc Pilipili inazidi kuimarika baada ya kupata ajali siku ya jumanne akiwa Mkoani Shinyanga.

Ambapo awali zilitoka habari kuwa mchekeshaji huyo yupo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu akisubiria kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha kutokea ajali hiyo ambapo alieleza kuwa Mc Pilipili alikuwa akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya mkoani humo.

LIVE: Uzinduzi wa mradi wa kulijengea uwezo Bunge
Manji afutiwa kesi ya uhujumu uchumi