Takriban watu 27 wamekufa baada ya kutokea maporomoko ya ardhi yalioikumba sehemu moja ya ya barabara kaskazini-magharibi mwa Colombia.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Colombia, Gustavo Petro amesema vifo hivyo vimetokea katika eneo la Pueblo Lico, baada ya vyombo vya usafiri kusombwa na maporomoko hayo.
Hata hivyo, Serikali ya Colombia imesema kipindi hiki cha mvua ni kibaya kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 40, hali ambayo imesababisha vifo vya zaid ya watu 270.
Mabadiliko ya hali ya hewa, uwepo wa vita nchini Ukraine na athari za Uviko-19 umeathiri maisha ya watu wengi Duniani kiuchumi na kiafya, huku wengi wakipoteza maisha.