Watawala wa kijeshi nchini Sudan na viongozi wa kiraia wametia saini ya makubaliano ya awali ya kumaliza mzozo mkubwa wa kisiasa unaoiandama nchi hiyo ya Afrika tangu kutokea mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja uliopita.

Mkataba huo, umesainiwa na mkuu wa utawala wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan, Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia cha RSF, Mohamed Hamdan Dagalo, na wawakilishi wa makundi ya kiraia ikiwemo yaliyoondolewa wakati wa mapinduzi mwaka jana 2021.

Makubaliano hayo, yanaweka msingi wa kuundwa kwa serikali ya mpito ya kiraia na yatafuatiwa na majadiliano mapana juu ya masuala mengine muhimu ikiwemo uendeshaji uchumi na usimamizi wa fedha za umma.

Kutiwa saini makubaliano hayo, kunafungua njia za kuirejesha Sudan chini ya utawala wa kiraia, ambao uliosambaratika mwaka jana (2021), baada ya jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu.

KFA yakanusha kujiuzulu kwa Paulo Bento
262 jela miaka miwili kwa kuandamana