Watu wenye maambukizi ya homa ya nyani, wanaweza kuwaambukiza wengine siku nne kabla ya dalili kuanza kijitokeza, huku kukiwa na mashaka kwamba zaidi ya nusu ya maambukizi huenda yakatokea katika kipindi cha sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, na ambao bado haujathibitishwa umeeleza kwamba maambukizi mengi ya homa ya nyani hayawezi kuzuilika kwa kuwaomba wagonjwa kujitenga mara wanapoanza kuona dalili.
Utafiti huo mpya, ulichapishwa katika jarida la afya la BMJ la nchini Uingereza ambali Taifa la kwanza kubaini visa vya maambukizi ya homa ya nyani nje ya Afrika.
Shirika la kimataifa la afya Ulimwenguni WHO, limesema watu 36 wamekufa na zaidi ya 77,000 wameambukizwa maradhi hayo tangu mwezi Mei, 2022 wakati virusi vya homa hiyo vilipoanza kusambaa ghafla katika mataifa ya Afrika ya Magharibi.