Nchini Tanzania, mabalozi wa Uingereza na Marekani wametoa salamu za pole kwa Watanzania na familia ya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustine Mahiga baada ya kifo chake kilichotokea leo Jijini Dodoma.

Ubalozi wa Marekani umetoa pole kwa familia ya Mahiga na taifa kwa ujumla kwa kumpoteza mzalendo wa taifa, wamesema hayo kupitia ukurasa wao wa Twetter.

“Ubalozi wa Marekani umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Waziri Augustine Mahiga. Tunatoa pole na rambirambi zetu kwa familia ya Mh. Mahiga na kwa taifa” umeandika Ubalozi wa Marekani

Ubalozi wa Uingereza nchini umesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kuondoka kwa mwanadiplomasia mwandamizi na mwenye busara ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa uingereza.

Ikumbukwe Dk Mahiga amehudumu kwa muda mrefu kama mwanadiplomasia kabla ya umauti kumkuta akiwa nyumbani kwake.

Idadi ya Wachezaji wa kigeni: Molinga, Chirwa watoa ya moyoni
TP Mazembe yaigomea Al Ahly